Home KITAIFA MHANDISI MARYPRISCA: WANAWAKE KUCHANGAMKIA MIKOPO NAFUU YA HALMASHAURI WASIKUBALI KUPOTOSHWA

MHANDISI MARYPRISCA: WANAWAKE KUCHANGAMKIA MIKOPO NAFUU YA HALMASHAURI WASIKUBALI KUPOTOSHWA

Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Habari Mwasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mary Prisca Mahundi amewataka wanawake nchini wasikubali kupotoshwa kuhusu mikopo ya halmashauri inayotolewa bila riba kwani ipo na wapo wanaoendelea kunufaika nayo sawa na agizo na maelekezo ya serikali kwa halmashauri zote nchini.

Amesema hayo leo Disemba, 4 2024 wakati wa Hafla ya utoaji wa zawadi kwa wanawake hodari wa sekta mbalimbali nchini iliyoandaliwa na Taasisi ya Women Power For Development kwa Tuzo za mwaka 2024 SUMA JKT Mwenge jijini Dar es salaam.

Amesema wanawake watumie fursa zinazotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na mikopo nafuu isiyo na riba inayotolewa na halmashauri badala kukubali kupotoshwa kwa taarifa zisizorasmi na kushindwa kunufaika na mikopo hiyo.

Amesema wanawake wasishindwe kuendeleza familia zao na aifa kwa ujumla kwa kukosa mitaji serikali inatoa mikopo nafuu isiyokuwa na riba ambayo imeandaliwa na serikali maalumu kwaajili yao “Mikopo nafuu ya Halmashauri ipo na wapo wanaoendelea kunufaika na mikopo hiyo hapa nchini”

“Kopa kwa wakati na mkiwa na malengo mahususi ya matumizia ya mikopo hiyo huku m kizingatia kurejesha vizuri kwa wakati itawaongezea kuaminiwa zaidi na mtapewa mikopo zaidi na wengine pia watakopeshwa,”amesema

Amefafanua kuwa Wanawake wasiogope kufuata taratibu zilizowekwa na serikali kwani mikopo ya Halmashauri inayotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Halmashauri nchini inalengo la kuwakwamua wanawake, vijana na watu wenye ulemavu nchini kwa kuwapa mitaji au kukuza mitaji yao ili kuhimarisha biashara zao.

“Nendeni mkapate elimu katika ya namna ya kupata mikopo hiyo kwa wakurugenzi wa Halmashauri kupitia idara ya Maendeleo ya jamii mkajieleze lengo la mikopo mnayotaka watawapa,”amesema.

Amesisitiza kuwa na nidhamu ya fedha baada ya kuchukua mikopo hiyo kwa kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa malengo waliyojiwekea na kusema fedha hizo sio za kununua khanga na vitenge bali ni kwaaili ya kukuza mitaji yao ilikukuza na kuendeleza biashara zao.

Mhandisi Mary Prisca amewasihi wanawake hao kutumia Umoja Ili kuweza kunufaika Kwa kuandika andiko na kupata Mikopo mbalimbali inayotolewa na Halmashauri Nchini

“Nidhamu ya fedha ni muhimu kwani wanawake ndio kundi lenye majukumu mengi katika familia lakini kwa mikopo hiyo wataweza kupunguza ukali wa maisha,” amesema.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewataka wanawake kuwa na tabia ya kujiwekea akiba katika kila wanachopata ikiwa ni pamoja na kutumia vizuri fedha kwa malengo bila kuzalau kile wanachopata hata kama ni kidogo “Ni lazima wanawake tusimamie malengo yetu katika maisha”

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Women Power For Development WPD Vaileth Konyani amesema taasisi hiyo inaibua vipawa na kutoa tuzo kwa wafanyabiasha na wazalishaji wadogo wasio na majina ili kuwatia moyo waendelee kufanya vizuri.

Amesema wamefanikiwa kuwakusanya makundi mbalimbali ya wanawake wakiwemo wajane na Kuwapa mafunzo kwa njia ya mitandao ya kjamii na ana kwa ana Ili waweze kuondokana na dhana ya kujiona wanyonge katika harakiti zao za uzalishaji Mali wa kila siku ambapo wamewafikia wanawake zaidi ya 10,000.

Akizungumzia uzinduzi wa Kikundi cha VICOBA Women Power For Development Vaileth amesema VICOBA hivyo vya wanawake wa mikoa mbalimbali nchini chenye jumla ya wanachama thelathini wenye lengo la kuwezeshana kiuchumi pia kuisaidia jamii hususani vijana na wanawake Katika nyanja mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here