Home AFYA LILIANROSE AIBUKA KIDEDEA KATIBU MSAIDIZI BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI.

LILIANROSE AIBUKA KIDEDEA KATIBU MSAIDIZI BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI.

Dar es Salaam

WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila limemchagua Lilianrose Fedrick kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza hilo kwa kupata kura 125 kati ya kura 241 zilizopigwa.

Katika uchaguzi huo uliofanyika mapema leo kwenye kikao cha 29 cha Baraza hilo, Lilianrose amemshinda Hilda Kajia aliyepata kura 114 ya kura zote ambapo kati ya kura hizo kura 2 zimeharibika.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Vaileth Gidion amesema uchaguzi huo umefanyika kufuatia kuunganishwa kwa Baraza la MNH-Upanga na Mloganzila na ambapo katibu anatoka Muhimbili Mloganzila hivyo katibu msaidizi lazima atoke Muhimbili-Upanga.

Vaileth amewakumbusha wajumbe kuwa vikao vya baraza vinatumika kujadili hoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji ambao utasaidia kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye malengo ya taasisi kwa ujumla.

Naye, Katibu Msaidizi aliyechaguliwa Lilianrose amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumchagua na kuongeza kuwa atashirikiana nao katika kupokea maoni, kero na ushauri ambapo pia atazifikisha kwenye uongozi kwa ajili ya ufumbuzi na utatuzi wa hoja hizo.

Vikao vya Baraza la wafanyakazi hufanyika mara mbili kwa mwaka, ambapo kikao cha 29-kina ajenda 12, baadhi yake ni kupokea mada kutoka kwa wataalam, kupitia mpango wa bajeti wa hospitali mwaka 2024/2025, kupokea mrejesho wa uchunguzi wa afya za watumishi pamoja na kupitia na kujadili mafanikio ya utekelezaji wa mpango kazi, kusoma na kujadili mizania ya mahesabu ya mwaka 2023/2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here