Dodoma
MBUNGE wa Kigamboni Dk.Faustine Ndugulile amefariki dunia usiku wa jana nchini India alipokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa leo Novemba,27 2024 na Bunge kupitia Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson imesema Ndugulile ambaye pia ni Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika amefariki dunia Novemba 27
“Nasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugullle kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu alaze roho ya marehemu mahall pema peponi,” amesema.
Amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.