Home KITAIFA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA SABA WA JUMUIYA YA MAMLAKA...

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA SABA WA JUMUIYA YA MAMLAKA ZA USIMAMIZI WA USAFIRI MAJINI AFRIKA

Dar es Salaam

TANZANIA inategemewa kuwa mwenyeji katika kutan meteuliwa kuwa nchi mwenyeji wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Novemba 29 hadi Desemba, 1 2024.

Mkutano huo unatarajia kufanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam unandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Taarifa iiiyotoewa leo Novemba, 25 2024 na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini barani Afrika huku kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini na kuongeza ushirikano baina ya nchi wanachama.

“Mkutano huu utatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama na mazingira ya usafri majini, pia, watapata fursa ya kuingia makubaliano ya kibiashara pamoja na kuanzisha mitandao na ushirikiano katika uendeshaji masuala mbalimbali yanayohusiana na fursa za uchumi wa buluu,” amesema.

Mkutano huu wa kihistoria utafunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (MO), Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini,

“Ushiriki wa Dominguez ni heshima kubwa kwa Tanzania hasa kipindi hiki tunapotekeleza Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu, ambapo kama nchi tumebainisha masuala ambayo Serikali kwa kushirikiana na wadau, kuhakikisha nchi inanufaika na fursa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu,”amesema.

Amesema washirki wengine ni viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, zipatazo 50 ambazo zina bahari, maziwa na mito na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa.

Ameongeza kuwa Tanzania itaendelea kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji zinazohusiana na utumiaji wa rasilimali za bahari na maziwa pamoja uchukuzi ili kukuza uchumi wa buluu, kufanya tafiti na kuwekeza katika uvunaji wa rasilimali bahari na maziwa Zitakazosaidia kuongeza UweZo wa endelevu Serikali kuwahudumia wananchi na kuwaleta maendeleo.

Ametoa wito kwa wadau wote wa sekta ya usafiri majini, wakiwemo wasafirishaj, wamiliki wa vyomnbo vya usafirishaji majini, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa Serikali kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huu muhimu ili kuunga mkono juhudi za Serikali Katika kuimarisha usafiri wa majini hapa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika: Ushirikiano katika Teknolojia na Ubunifu ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha usalama, na mazingira ya sekta ya usafiri majini kwa mustakabali endelevu”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here