Home KITAIFA THDRC YASISITIZA SERIKALI KUWEKA MFUMO WA MABORESHO YA USIMAMIZI WA MAJENGO NA...

THDRC YASISITIZA SERIKALI KUWEKA MFUMO WA MABORESHO YA USIMAMIZI WA MAJENGO NA MAJANGA

Dar es Salaam

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC) umesisitiza uhitaji wa serikali kuweka mfumo,utaratibu na mathubuti wa usimamizi na ufuatiliaji wa uhai wa majengo hasa ya umma na biashara yanayo jumuisha idadi kubwa ya watu ili kuepuka athari zilizotokea jengo la kariakoo.

Akizungumza leo Novemba,18 2024 jijini na waandishi wa Habari, Mratibu wa Mtandao huo, Wakili Onesmo Ole Ngurumwa amesema umefika wakati kwa mamlaka mbalimbali za serikali zinazohusika na usimamizi wa vibali kufanya ufuatiliaji kwenye majengo hayo.

Amesisitiza kuna uhitaji wa Taifa kuboresha mifumo ya utatuzi wa majanga.

“Uhitaji wa maboresho ya sheria inayosimamia majanga ili kuwe na kamati za kudumu zitakazokuja na suluhu za muda mrefu kutatua majanga na kuondokana na muundo wa kuwa na kamati zinazokutana baada ya matukio,” amesema

Amesema Tanzania kuna sheria ambayo inasimamia majanga ambayo ilitungwa mwaka 2015 na inaendelea kufanyiwa maboresho mara kwa mara.

Wakali Ole Ngurumwa amesema suala la majanga ni endelevu hivyo wanapendekeza kuwe na kamati ya majanga ya kudumu iwe ya kufutilia, kujua na kubatili majanga nchini na kutoa elimu kwa wananchi.

Akizungumzia kuhusu changamoto mbalimbali ambazo zinejitokeza kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa amesema Novemba, 20 wanatarajia kuanza kampeni hivyo asilimia 99 serikali ya mtaa inaunganisha jamii na wananchi.

“Mtandao huu umehimiza uhitaji wa kufanyika kwa Uchaguzi huru na wa haki kupitia mifumo sahihi ya usimamizi wa uchaguzi,” amesema.

Aidha Wakili Ole Ngurumwa amesema wananchi wa Tarafa ya Ngorongo wanaanza kuthaminiwa baada viongozi mbalimbali wa Serikali kwenda kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao.

“Kufuatia maagizo la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yametekelezwa kwa ujumla ikiwemo viongozi kuweka kambi ya kufanya tathmini ya mahitaji yote,”amesema.

Amesema wanahitaji shilingi bilioni 2 kwaajili ya kufanya ukarabati wa maeneo ya shule, zahanati, barabara pamoja na huduma za msingi hivyo kuna fedha zilienda kwenye akaunti ya vijiji na shule wao walijionea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here