Home KITAIFA WAZIRI MKUU AAGIZA JESHI LA POLISI LIMKAMATE “NIFFER” KWA KUCHANGISHA FEDHA

WAZIRI MKUU AAGIZA JESHI LA POLISI LIMKAMATE “NIFFER” KWA KUCHANGISHA FEDHA

Na Sophia Kingimali.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagizaJeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka za kumsaka mfanyabiashara Jennifer Jovin “Niffer” kwa kuendesha zoezi la kukusanya michango bila ya kuwa na kibali kufuatia kudondoka kwa ghorofa kariakoo.

Hayo ameyasema leo Novemba, 18 Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza wananchi zoezi la kuaga kitaifa miili ya watu 16 waliofariki katika ajili ya kudondoka kwa ghorofa iliyotokea Novemba 16,katika eneo la kariakoo jijini Dar es salaam.

Amesema Jeshi la polisi linapaswa kumtafuta popote alipo ili aweze kueleza ametoa wapi kibali cha kufanya zoezi hilo na amekusanya kiasi gani? tena kwa kutumia namba yake binafsi.

“Nitumie nafasi hii kuwaonya wanaotumia fursa ya tukio hili kukusanya michango ya watu bila ya kuwa na kibali jeshi la polisi linapaswa kuwatafuta wote wanaofanya zoezi hilo maana huo ni wizi wa pesa za watanzania nimeambie huyu Jennifer Jovin kama ananisikia aende mwenyew kituo cha polisi kabla jeshi hilo alijamtafuta”,amesema Majaliwa.

Aidha ametoa rai kwa wadau mbalimbali na walioguswa na tukio hili kutoa michango yao kupitia akaunti ya maafa iliyopo benki kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here