-Ataja idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha kwa mujibu wa taarifa za kidakitari
-Asema juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea taarifa nyingine itatolewa saa 4:30 usiku
Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema zoezi la uokoaji halijasimama kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, ukweli ni kwamba zoezi linaendelea hakuna kilichosimama ndio maana viongozi wote tuko hapa.
Aidha toka uokoaji uanze hadi kufikia saa 11:00 jioni watu 70 wameokolewa wakiwa hai lakini kwa mujibu wa taarifa za kidaktari watu 4 tu ndio wamepoteza maisha
Pia Chalamila amevishukuru vikosi mbalimbali na wadau wingine ambao wanaendelea kutoa misaada ya hali na mali ili kufanikisha shughuli nzima ya uokozi.
Vilievile amesama taarifa kwa umma itaendelea kutolewa kadri zoezi hilo linavyoendelea aidha ifikapo saa 4:30 usiku atatoa tena taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya uokoaji.