Home BIASHARA TCB BENKI KUUNGA MKONO MALENGO YA RAIS DK.SAMIA KWA KUTOA KIASI CHA...

TCB BENKI KUUNGA MKONO MALENGO YA RAIS DK.SAMIA KWA KUTOA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 300 KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

Dar es Salaam

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imejizatiti kuunga mkono malengo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kukuza uchumi nchini kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa wafanyabiashara wadogo na wakati kuinuka kiuchumi.

Akizungumza leo Novemba,13 2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Biashara kwa Wateja wadogo na Kati wa TCB, Lilian Mtali amesema dhamira ya benki hiyo ni kushiriki kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

Amesema benki hiyo imekuwa sokoni kwa miaka 99 hivyo wamedhamiria kupeleka mbele gurudumu la maendeleo nchini kwa kuwa vinara wa kuleta suluhu kwa wajasiriamali wadogo na kati kufanya biashara kwa urahisi popote.

“Tukiwa kama benki ya serikali tumeona tuwe vinara katika kuleta ‘solution’ kuhakikisha mjasiriamali mdogo anakua katika ufanyaji biashara kwa kufanya malipo kwa urahisi popote alipo,” amesema.

Amesema katika kuwainua wafanyabiashara hao mpaka sasa kiasi cha sh. bilioni 300 kimetolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara wadogo na kati na shilingi bilioni 250 kwa mfanyabiashara mmoja mmoja.

“Tumeamua kuja na huduma mpya ya ‘Lipa Popote’ ambayo ni suluhisho la malipo lililobuniwa kurahisisha miamala kwa wajasiriamali wadogo na kati (SMEs) na wamiliki wa biashara na huduma hiyo inawawezesha wateja kupokea malipo moja kwa moja katika akaunti zao kupitia namba moja ya iitwayo Lipa Popote,” alieleza.

Lilian amesema wafanyabiashara wadogo na kati ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hivyo suluhisho hilo linalenga kurahisisha mchakato wa malipo kwa wamiliki wa biashara na kuwawezesha kupokea malipo papo hapo kwa usalama.

Amesema njia hiyo ya malipo inatarajiwa kubadilisha namna biashara ndogo zinavyofanya kazi na kurahisisha miamala ya kifedha.

“Kwa kuzindua suluhisho la kidijitali la malipo kama vile Lipa Popote, tunaboresha kikamilifu malengo ya Tanzania ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wafanyabiashara, watu binafsi na jamii ambazo hazijafikiwa bado,” amesema.

Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali na Ubunifu wa benki ya TCB, Jesse Jackson amesema benki hiyo imekusudia kukuza ubunifu unaogusa maisha ya Watanzania kwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo na kati kupata suluhisho bora la malipo bora, rahisi na salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here