Home KITAIFA LATRA IMETOA KADI 174 ZA USAJILI WA WAHUDUMU WA MABASI YA ABIRIA

LATRA IMETOA KADI 174 ZA USAJILI WA WAHUDUMU WA MABASI YA ABIRIA

Dar es Salaam

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) imetoa kadi 174 za usajili wa wahudumu wa mabasi ya abiria ya masafa marefu ambao wamekidhi vigezo na kusajiliwa.

Akizugumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Novemba,12 2024 Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema utoaji wa kadi hizo kwa wahudumu kuna akisi kiu ya LATRA ya kutaka kuona huduma bora ya usafirishaji nchini.

“Hafla hii ina tafsri ndoto ya Serikali ya awamu ya sita namna ya kuboresha maslahi yenu kama watoa huduma pamoja na kuboresha sekta mzima…pia inatoa tafsiri na Mpango kababe wa kukabiliana na ajali za barabarani,”amesema

Amesema hatua ya ugawaji kadi kwa wahudumu hao inaziilisha umakini wa Serikali katika kuongeza ajira katika Nchi na kutoa heshima wa kada ya wahudumu ili waweze kutambulika rasmi.

Aidha ameipongeza Bodi na Menejimenti ya LATRA kwa kuhakikisha suala la ubora wa huduma usafiri linapewa kipaumbele na uzito ili kusimamia
upitishwaji wa wadau.

Pia ametoa wito kwa wahudumu hao kuyatumia vyema mafunzo waliopata na kuwa mfano bora kwa wahudumu wengine.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (LATRA),Johansen Kahatano amesema hatua ya kutoa kadi za usajili wa wahudumu wa mabasi ya abiria ulianza na kuandaa mwogozo wa mafunzo ambapo Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) na Chuo Cha Usafirishaji (NIT)ndio waliandaa mtaala.

Amesema kadi hiyo ni zaidi utambulisho kwani itakuwa ikitumika katika matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya malipo .

“Kadi hii itakuwa na manufaa makubwa Kwa wahudumu kwani wataweza kutambulika kwani kadi hiyo ni zaidi ya utambulisho,”amesema.

Aidha ametoa wito kwa wahudumu wa mabasi ambao awajapata mafunzo na kusajiliwa kuchangamkia fursa hiyo kwani itafika wakati wasiokuwa na kadi awataweza kutambulika.

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa LATRA,Ahmed Mohamed Ame alisema hadi kufikia Oktoba mwaka huu zaidi ya wahudumu 700 walipewa mafunzo kati yao 174 ndio waliokidhi vigezo na kusajiliwa.

“LATRA inatekeleza majukumu yake Kwa mujibu wa kifungu cha (5) (1) cha Sheria ya Mamlaka ya Ardhi Usafiri Ardhini sura ya 413 ambapo miongoni mwa majukumu hayo ni kusajili wahudumu na kuthibitisha madereva,”amesema.

Aidha ametaja faida za wahudumu kuudhuria mafunzo na kusajiliwa na LATRA ni pamoja na kuboresha huduma za Usafiri Ardhini, wahudumu kufanya kazi kwa weledi, umakini na ufanisi zaidi pamoja na kulinda mitaji ya wamiliki wa vyombo na vipato vya wahudumu.

Kwa upande wake mmoja wa wahudumu waliopewa kadi hizo Gift Manege ameipongeza LATRA kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika majukumu yao ya kazi.

Aidha amewaomba wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuwapatia mikataba ya kazi ili waweze kujikwamua kimaisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here