Home BURUDANI TANZANIA NA KUBA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA SANAA

TANZANIA NA KUBA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA SANAA

Cuba

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Tabia Maulid Mwita wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Utamaduni wa Jamhuri ya Cuba Alpidio Alonso Grau Novemba 9, 2024 Jijini Havana.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili juu ya kuanzisha mashirikiano katika sekta ya Sanaa hususani filamu na muziki.

Kwa upande wa filamu wamesema kuwa, ni vyema kuandaa filamu zitakazo onesha jinsi Tanzania na Kuba zilivyosaidia kupatikana kwa uhuru wa nchi nyingine za Afrika.

Aidha, nchi hizo mbili zitaanzisha ushirikiano katika Sanaa ya muziki ambapo watabadilishana uzoefu wa kufundisha muziki na kualika wasanii kutoka nchi zote mbili kutumbuiza katika kalenda za matukio ya Sanaa ya nchi zote mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here