Home KITAIFA MAWAZIRI WATATU WAJADILI MAENDELEO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

MAWAZIRI WATATU WAJADILI MAENDELEO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

Na Saidina Msangi, Dodoma

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Madini Antony Mavunde wamekutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya Sekta ya madini na uwekezaji ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Japhet Justine na wajumbe wengine kutoka Wizara hizo tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here