Home KITAIFA NAIBU KATIBU MKUU AZINDUA PROGRAMU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA WIZARA YA...

NAIBU KATIBU MKUU AZINDUA PROGRAMU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Maduhu Kazi amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kutambua umuhimu wa Mazoezi katika kuimarisha afya na kuwaleta watu pamoja hivyo kuimarisha upendo na mshikamano baina ya Watumishi.

Dk. Maduhu ameyasema hayo alipokua akizindua programu ya Mazoezi kwa Watumishi wa Wizara hiyo iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Dodoma Mlimani Novemba 5, 2024

Naibu Katibu Mkuu ameipongeza Menejimenti ya Wizara kwa kutoa fursa hiyo itakayosaidia kuimarisha na kuboresha afya za watumishi kupitia Mazoezi, aidha amewasisitiza watumishi Watumishi kutumia nafasi hiyo kushiriki kwenye Mazoezi hayo yatakayokuwa yakifanyika mara mbili kwa wiki kila siku ya Jumanne na Alhamisi kuanzia saa 10 Alasiri

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwasisitiza Watumishi wote kushiriki Mazoezi haya kila wiki kwa watumishi waliopo hapa Dodoma na kwa wale walipo nje ya Dodoma,” amesema Dk. Maduhu

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watumishi kuhusu Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba, 27 2024 hivyo aliwasihi Watumishi wajitokeze Kwa wingi kupiga kura kwani ni haki yao ya msingi

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Hilda Tegwa ametangaza rasmi maeneo ya kufanyia Mazoezi hayo.

“Kwa Watumishi waliopo Ofisi za Wizara Mtumba watafanya mazoezi katika eneo la viwanja vya ofisi ya Mtumba na kwa waliopo Kambarage Tower watafanya Mazoezi hayo katika viwanja vya Shule ya Msingi Dodoma Mlimani, Watumishi waliopo nje ya Dodoma watafanya Mazoezi katika viwanja vilivyopo Maeneo yao kazini kwao,” amesema Tegwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here