Home KITAIFA MAGOTI :VIJANA JESHI LA AKIBA MSIJIINGIZE KWENYE MAKUNDI YA KISIASA

MAGOTI :VIJANA JESHI LA AKIBA MSIJIINGIZE KWENYE MAKUNDI YA KISIASA

Na Mwandishi wetu

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti ametoa wito kwa Vijana wa Jeshi la Akiba kutojiingiza kwenye makundi ya siasa mara baada ya kuhitimu Mafunzo yao bali kufata vifungu vya sheria za Jeshi hilo la Akiba.

Mkuu wa Wilaya huyo ameyasema hayo Novemba, 1 2024 wakati wa kufunga mahafali ya Miezi Minne kwa Askari wa Jeshi la Akiba(Mgambo),Mkoani Pwani amesema Askari hao wanapaswa kujiadhari kwa kiasi kikubwa na maneno ya wanasiasa kwani ni rahisi kuwapotosha

“Ninaomba niwaase ,Jeshi la Akiba mtambue mpo chini ya vifungu vya Sheria hivyo msikubali kutumika kisiasa kwa namna yoyote ile hakikisheni mnalinda
heshima za Jeshi,viapo vyenu,nidhamu mliyofundishwa na Uzalendo wa taifa letu,”amesema.

Amesema askari hao wanapaswa kusimamia Taifa ,Mikoa na Wilaya ipasavyo na kuwa macho kwa serikali katika kutoa taarifa za kihalifu hususan za ubadilifu wa maliasiri za nchi na nyara za serikali.

“Popote mtapoona zinatumika vibaya katika maeneo mtakayoishi, mtatoa taarifa juu ya mtu yoyote ambaye anahatarisha hali ya usalama katika maeneo yenu katika uchochezi wa masuala ya kisiasi na ugaidi,”amesema.

Kwa Upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Kisarawe,Meja SILVERY Mabubu amesema miongoni mwa changamoto zinazowakumba katika mafunzo hayo ni pamoja na ufinyu wa bajeti uliopo.

“Tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa uongozi wake kutusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo suala la usafiri na mafuta pindi ya Kozi hii ikiwa inaendelea,”amesema.

Amesema wanapendekeza halmashari ianze kuwazingatia katika bajeti hata wakikusanyiwa kiasi cha fedha kidogo kidogo hadi hapo wanapoanza kozi nyingine itakuwa inawasaidia katika kupata zana za kufundishia na maandalizi ya porini.

Kozi hiyo imefanyika kwa muda wa wiki 16 katika Kata ya Manerumango iliyopo Wilayani Kisarawe Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here