Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani Oktoba, 30 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia mjadala kuhusu Kilimo Barani Afrika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation Oktoba, 30 2024.