📌 Asema Rais Samia anataka Ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi
📌 Asisitiza utendaji kazi umuangalie Mtanzania wa kawaida anayeitegemea Serikali kubadili maisha
📌 Ataka Watendaji waache alama ya kazi, si kulinda vyeo
Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi ikiwemo za umeme, mafuta,
na Nishati Safi ya Kupikia.
Amesema hayo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa Kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi.