Dar es Salaam
WAZIRI wa Kilimo,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shemata Shame Khamisi amesema Serikali ya Zanzibar imetekeleza afua mbalimbali katika kuhakikisha tasnia ya kuku inakua na kuleta tija kwa kuwajengea uwezo wa wataalamu wa mifugo wa ndani katika mbinu za kisasa za ufugaji bora na udhibiti wa magonjwa.
Pia kuweka mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ya kuku na ndege wafugwao ili kudhibiti milipuko ya magonjwa pamoja na kuimarisha utekelezaji wa afua za Afya.
Ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2024 jijini Dar es salaam, Waziri Khamisi wakati akihitimisha Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na Ndege wafugwao kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
“Mkakati hiyo ni Kuanzisha mashamba ya kuku, Uwekezaji katika maeneo ya kutotoleshea vifaranga vya kuku,Kuanzishwa kwa kiwanda kipya cha vyakula vya mifugo,Kuanzishwa kwa machinjio mapya ya kuku, Kuwekeza katika maabara ya mifugo na uwezo wa uchunguzi, pamoja na uzalishaji wa chanjo za mifugo pamoja na Kuanzisha vituo vya utafiti wa kuku” amesema Khamisi
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeweka mikakati mbalimbali katika kuhakikisha Tasnia hii ya kuku na ndege wafugwao inakua na kuchangia zaidi katika ajira, uchumi na kuimarisha usalama wa chakula na lishe.
Ameongeza kuwa kuna Mikakati ambayo serikali ya zanzibar inatekeleza pamoja na Kufungamanisha kanuni na viwango vya ufugaji kuku katika nchi za SADC ili kuwezesha biashara za kikanda na kuhakikisha usalama wa mazao ya kuku na bidhaa zake.
“Kuanzisha programu za pamoja za utafiti kati ya nchi za SADC ili kushughulikia changamoto zinazofanana zikiwemo udhibiti wa magonjwa, mbinu na teknolojia za kuboresha ufugaji. Kuendeleza programu za mafunzo za kikanda kwa wafugaji, madaktari wa mifugo, na wafanyakazi wa ugani ili kuongeza ujuzi katika usimamizi wa kisasa wa kuku na ustawi wa wanyama,” ameeleza.
Aidha ametoa rai kwa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha tasnia ya kuku na ndege wafugwao, ili kupunguza ma kuondoa changamoto, vikwazo vilivyopo katika tasnia ya kuku.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi Tanzania wa Shirika la Shirika la Uboreshaji wa Kijana Tanzania (AGRA), Vianey Rweyendela amesema Azimo la kwanza ni kuwa Mpango mmoja katika nchi za SADC ambao utatengeneza mashirikiano ya maendeleo ya maswala ya Kuku na Ndege wafugwao.
“Kitakachofanyika tumeangalia kila nchi inafanya nini na iko wapi na kama nchi inapungufu kitu gani inaweza kuwa ni tatizo kwa nchi moja na kuws Fursa kwa nchi nyingine, lengo ni kutaka kupunguza uagiziji wa kuju na bidhaa zake kutoka nje ya eneo la SADC,” amesema.
Ameongeza kuwa asilimia 50 bidhaa za kuku na kuku wenyewe wanaotumia katika nchi za SADC wanatoka nje, wanakwenda kwenye upotevu wa fedha zakigeni ambazo zingetumika kwenye vitu vingine.
Aidha amesema kuwa wamekubaliana kuwa na mipango mimoja itayakuwa chini ya SADC itakuwa inangazia maswala ya yote kuku na ndege wafugwao.
“Umuhimu wake ni kwamba tutaongeza ustawi wa wakulima kwa kuwaongezea tija pamoja na Faida, lakin pia ustawi wa jamii, tutaongeza kipato kutoka nje na ni fursa kubwa sana kwa Tanzania ambayo emekuwa mwenyeji,”amesema.