Home KITAIFA RAIS DK. MWINYI:MAFANIKIO YA UTALII YANAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

RAIS DK. MWINYI:MAFANIKIO YA UTALII YANAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

Dar es Salaam

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DK. Hussein Ali Mwinyi, amesema mafanikio makubwaYanayopatikana chini kupitia sekta ya utalii yanaitangaza Tanzania kimataifa na kuitambulisha duniani kuwa nchi ya kwanza AfrikaKwa ongezeko la idadi ya watalii kwa mujibu wa Shirika la Utalii Duniani na inashika nafasi ya sita duuniani nl

Hayo ameyasema Leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – s!te 2024) ambalo limeanza oktoba 11, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City, ambalo limewakutanisha wanunuzi wa bidhaa za utalii, Waoneshaji, Wawekezaji na wadau mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ya Tanzania.

Ameiipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa jitihada kubwa za kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii katika kipindi kifupi cha Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Juhudi hizo za  Rais Dk. Samia, idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Nchi yetu imekua kwa kasi sambamba na ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya utalii. Mathalan, hadi kufikia mwezi Agosti, 2024 Tanzania imepokea jumla ya watalii wa kimataifa 2,026,378 ikiwa ni takwimu za juu kabisa kuwahi kufikiwa katika historia ya Nchi yetu. Pia, mapato yatokanayo na sekta ya utalii yamefikia Dola za Marekani bilioni 3.5,” amefafanua Dk. Mwinyi.

Amesema mafanikio hayo ji juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundombinu ya utalii ikiwemo kuendelea kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania ( ATCL).

Dk.Mwinyi amesema Pamoja na kuhamasisha mashirika mengine ya ndege ya kimataifa kuanzishwa safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na nchi zenye masoko ya utalii.

Amesema sekta ya utalii imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania, huku ikichangia asilimia 17.2 ya Pato Ghafi la Taifa, asilimia 25 ya mauzo ya nje na kuzalisha ajira zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia mnyororo wake wa thamani. 

Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamewezesha nchi yetu kutambuliwa kimataifa na kupata tuzo mbalimbali ambapo taarifa iliyotolewa mwezi Septemba, 2024 na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism – World Tourism Barometer) ambapo inaonesha kuwa, Tanzania imeshika nafasi ya 6 Duniani na ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii.  

Miongoni mwa tuzo hizo ni zile zilizotolewa mwaka 2023 na World Travel Awards (WTA) ambao wameitambua Bodi ya Utalii Tanzania kama Africa’s Leading Tourist Board, Kisiwa cha Thanda Shunghumbili, Mafia kama World Leading Exclusive Private Island, Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kama Africa’s Leading Tourist Attraction.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasi na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana amesema sekta ya Utalii imekuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la taifa ambapo inachangia asilimia 17.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here