Na Shomari Binda-Simiyu
SHEKH wa mkoa wa Simiyu Issa Kwezi amewahimiza wazazi na walezi kuipa umuhimu elimu ya dini kwa kuwapeleka watoto madrasa.
Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 9 ikiwa ni wiki ya Maulid itakayofanyika jumamosi ya oktoba 12 kwenye uwanja wa CCM Bariadi.
Amesema mtoto anapopata elimu ya Dini anakuwa na na hofu ya Mwenyezi Mungu na hawezi kushiriki matukio yasiyofaa.
Shekh Kwezi amesema watoto wanapopelekwa kwenye elimu ya dunia watengewe muda wa kufundishwa pia elimu ya akhera yao.
Amesema mkoani Simiyu madrasa zipo na maustadh wakufundisha watoto wapo hivyo wapelekwe wakafundishwe elimu ya dini.
Amesema mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa kwenye jamii na elimu ya dini ndiyo itakayowaweka watoto kwenye mstari.
” Tukiwa tupo kwenye wiki ya Maulid nitoe wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto madrasa wakaijue dini yao.
” Elimu ya dunia inamanufaa na elimu ya akhera inamanufaa makubwa wazazi na walezi wasiache kuwapeleka watoto madrasa”,amesema.
Sherehe za Maulid kimkoa mkoani Simiyu zitafanyika jumamosi oktoba 12 ambapo wageni mbalimbali wamealikwa na mgeni rasmi atakuwa Mufti wa Tanzania Alhaj Dk.Abubakar Ally Zuberi.