Home KITAIFA VIJANA UVCCM MARA KUFANYA MATEMBEZI BUTIAMA HADI MWANZA KUMUENZI MWALIMU NYERERE

VIJANA UVCCM MARA KUFANYA MATEMBEZI BUTIAMA HADI MWANZA KUMUENZI MWALIMU NYERERE

Na Shomari Binda-Musoma

VIJANA zaidi ya 1000 wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) mkoa wa Mara watafanya matembezi ya kilometa kutoka Butiama hadi Mwanza kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza n leo oktoba 7 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) Mkoa wa Mara, Irene Moleli amesema vijana wanaendelea vizuri na kambi iliyopo chuo cha ufundi Veta wilayani Butiama na wapo tayari kwa matembezi hayo.

Amesema matembezi hayo yatakayoanza jumatano ya oktoba 9 yana lengo maalum ya kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Irene amesema Baba wa Taifa amelifanyia Taifa mambo mengi mazuri hivyo kama vijana lazima wamuenzi kwa hayo aliyoyafanya.

Amesema moja ya mambo ambayo vijana hao wanafundishwa kwenye kambi hiyo ya mkoa ni uzalendo ambao Mwalimu Nyerere alikuwa akihusisitiza enzi ya uhai wake.

Katibu huyo amesema vijana waliopo kambini wapo na afya njema na wanaendelea na mafunzo kabla ya kuanza matembezi hayo.

“Wakufunzi kutoka makao makuu na wa hapa mkoani wanaendelea kuwapika vijana kuwa wazalendo na masuala mengine na wanaendelea vizuri.

” Matembezi yetu yataanzia hapa Butiama na tutatembea hadi mkoani Mwanza kushiriki wiki ya vijana na kilele cha mwenge wa Uhuru,”amesema.

Kwa upande wao vijana wanaoshiriki kambi hiyo wamesema wanajifunza mambo mengi mazuri ambayo yamewafanya kuwa wa tofauti kwa kuijua misingi ya uzalendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here