Zanzibar
LEO Oktoba, 72024 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia leo ameshikri katika uzinduzi wa Programu maalumu ya mafunzo ya Airtel Africa Fellowship Program inayoendeshwa kwa mashirikiano baina ya Taasisi ya Teknolojia ya India Madras, Kampasi ya Zanzibar (IITMZ) na Taasisi ya Airtel Africa Foundation.
Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 jumla ya wanafunzi kumi kutoka nchi za Tanzania, Kenya na Zambia walioanza masomo yao ya Shahada ya Kwanza katika fani za Sayansi ya Data na Akili Bandia watafaidika na program hiyo.
Shughuli hiyo iliyofanyika katika kampasi za IITMZ imehudhuriwa na viongozi, wazazi wa wanafunzi na wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu nchini.