Home MICHEZO MSHIKAMANO FC YATINGA FAINALI POLISI JAMII CUP 2024 MUSOMA

MSHIKAMANO FC YATINGA FAINALI POLISI JAMII CUP 2024 MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Mshikamano fc imetinga fainali ya michuano ya Polisi Jamii Cup 2024 Musoma kwa kuifunga timu ya Kigera fc kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4.

Dakika 90 za mchezo huo uliofanyika leo Septemba, 25 2024 kwenye uwanja wa Mara sekondari zilimalizika kwa timu hizo kufungana mabao 2-2

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo afisa habari wa timu ya Mshikamano Julius Silima amesema walistahili kuingia fainali kwa kuwa wana timu bora.

Amesema baada ya kuingia fainali wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanachukua ubingwa na kupeleka ng’ombe Kata ya Mshikamano.

Silima amesema mchezo dhidi ya Kigera ulikuwa mgumu na wachezaji wanastahili kupongezwa kwa ushindi walioupata.

Msemaji huyo wa Mshikamano amewashukuru mashabiki waliofunga safari hadi uwanja wa Mara sekondari na kuishangilia timu yao.

“Tunawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwakuoambana na kuweza kuibuka na ushindi dhidi ya timu ngumu ya Kigera.

” Mashabiki wetu pia ni watu wa kupongezwa baada ya kufunga safari kutoka Mshikamano kuja kuishangilia timu yao sasa tunasubili timu yoyote kwenye mchezo wa fainali “,amesema Silima.

Nusu fainali ya pili ya mashindano hayo itapigwa septemba 26 siku ya alhamis kati ya timu ya Mwigobero na Mara Sports.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here