Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo, wakati alipokuwa anawasili Uwanja wa Ndege wa Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024, kwa ajili ya kukagua jengo jipya la kuongozea ndege katika uwanja huo, ambalo linatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Septemba 23, 2024 Mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akiwatambulisha Maafisa wa TCAA kabla ya kutoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine uwanjani hapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Songea, Kasmiri Fortunatus, wakati Mkurugenzi Mkuu huyo alipokuwa analikagua jengo jipya la kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce. Jengo hilo pamoja na miradi mengine uwanjani hapo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akitoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege, katika uwanja wa ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine katika kiwanja hicho inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024.