Dar es Salaam
Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakijiandaa kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku na jeshi hilo kwa kile kinachotajwa kuwa taarifa za kiintelijeshia zilibaini kuwepo kwa nia ovu.
Kamanda wa Polisi kanda maalumuu ya Dar es Salaam Jumanne Murilo leo Septemba, 23 2024 ameviambia vyombo vya habari kuwa jumla ya watu kumi na nne wakiwemo viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu na Godbless Lema.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi viongozi hao wamekamatwa wakiwa wanahamasisha kufanyika kwa maandamano ambayo hayana kibali.
Kamanda wa jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema Polisi wanaendelea kusisitiza kuwa hakuna kibali cha kufanya maandamano hivyo wataendelea kuwakamata wote wanaohamasisha maandano hayo.
Hata hivyo, kamanda Murilo hajasema ni lini watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani.