Home KITAIFA MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS DK.SAMIA ALIPOTEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA YA...

MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS DK.SAMIA ALIPOTEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA YA MAJIMAJI

Matukio mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma leo Septemba, 23 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa Songea Mkoani Ruvuma. Rais Dk. Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Chifu Msaidizi wa Wangoni Nduna Songea Mbano ambaye pia alinyongwa na kukatwa Kichwa na Wajerumani mwaka 1906. Rais Dkt. Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here