Home KITAIFA BASHE ATEMBELEA MAGHALA MBALIMBALI YA UHIFADHI NA UUZAJI MBOLEA

BASHE ATEMBELEA MAGHALA MBALIMBALI YA UHIFADHI NA UUZAJI MBOLEA

Ruvuma

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile na kutembelea maghala mbalimbali ya uhifadhi na uuzaji wa mbolea yaliyopo Songea mjini leo Septemba,22 2024.

Dhumuni kuu la ukaguzi huo kuona utararibu wa bei za jumla kabla ya gharama za usafiri. “Naielekeza Mamlaka ya Udhibitj wa Mbolea (TFRA) kuhakikisha inatoa mwongozo wa bei za jumla na reja reja kwenye kila kituo kinachouza mbolea nchini,” amesema Waziri Bashe.

Vile vile, Waziri Bashe ametembelea ghala la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililokarabatiwa kwa ajili ya kuhifadhi na kuuza mbolea za kupanda aina ya DAP na za kukuzia mazao aina ya UREA. Ghala linapatikana katika eneo la viwanda la Ruhuwiko, Songea mjini. Ghala lina ukubwa wa uwezo wa square metre 5000, kwenye ekari 16 na lina uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za mbolea. Ghala hilo litatoa huduma katika Mkoa wa Ruvuma na Wilaya zake zote.

Kwa nyakati tofauti, Waziri Bashe ameongea na Wafanyabiashara kujadiliana nao mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja ba bei wanazouza kwa wakulima.

“Nashauri mkae pamoja kuwa na uwiano wa bei ambayo haimuumizi mkulima na pia iwe bei yenye gharama za uhalisia,” amesema Waziri Bashe.

Ameielekeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kuhakikisha viuatilifu vinasambazwa nchini na kuimarisha mfumo wa kanzidata kuongeza kuwe na taarifa ya muuzaji na mnunuaji (traceability) na kuweka QR Code kwenye kila chupa / bidhaa.

Wafanyabiashara hao ni wa Mkoa wa Ruvuma, katika mauzo ya mbolea na mazao mbalimbali yakiwemo mahindi.

Aidha, Waziri Bashe ameomba wadanyabiashara hao endapo wapo tayari wajenge maghala ya tani elfu moja moja ndani ya Mkoa wa Ruvuma, ambapo Wizara itaingia nao mikataba kupitia Taasisi yake ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kukodi kwa ajili ya kuhifadhi nafaka hadi ata miaka 10.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here