Home KITAIFA KITUO CHA TARI NDENGU KUFUFULIWA

KITUO CHA TARI NDENGU KUFUFULIWA

Ruvuma

KITUO cha Utafiti wa Kilimo cha TARI kilichojengwa mwaka 1959 katika eneo la Ndengu, Wilayani Mbinga kwenye Mkoa wa Ruvuma kimeelekezwa kufufuliwa ili kianze shughuli za uzalishaji wa mbegu za ngano, tafiti za mbegu za mpunga na muhogo, pamoja na upimaji wa afya ya udongo.

Ameelekeza hayo Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliposimama kukikagua wakati wa ziara yake katika Wilaya za Nyasa na Mbinga Septemba,20 2024.

Waziri Bashe ameongeza zaidi kuwa Mkurugenzi wa TARI Uyole, Dk. Tippe ahakikishe Kituo hicho kitakufufuliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo (ASA) ili kuzalisha mbegu kwa wingi kusaidia wakulima wa Wilaya hizo mbili ambao wanafanya kilimo cha kahawa, mpunga, muhogo, michikichi, mahindi na mazao mengine.

Naye Dk. Tippe ameomba Watumishi wa tatu wa Kituo hicho wapatiwe pikipiki kusaidia usafiri; ambapo ombi hilo Waziri Bashe aliridhia na kuielekeza Wizara ya Kilimo iwapatie pikipiki tatu.

Aidha, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) nayo imeelekezwa kusaidia upatikanaji wa mbolea za ruzuku ili wakulima wa eneo hilo waweze kunufaika kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mbegu za ruzuku zisambazwe kwa wakulima na kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here