Home KITAIFA UCHUNGUZI WA KISAYANSI UMESAIDIA KUUNGANISHA WAHALIFU NA TUHUMA ZINAZOWAKABILI KIURAHISI.

UCHUNGUZI WA KISAYANSI UMESAIDIA KUUNGANISHA WAHALIFU NA TUHUMA ZINAZOWAKABILI KIURAHISI.

Dar es Salaam

JESHI la Polisi Nchini limeungana na wadau wengine dunia katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uchunguzi wa sayansi ya Jinai leo Septemba, 20 2024 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kurasini.

Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna Wa Polisi Uchunguzi wa Kisayansi, Mgeni rasmi katika halfa hiyo Naibu Kamishna wa Polisi, DCP. Mwamini Rwantale amesema hiyo ni mara ya kwanza kwa jeshi la Polisi kuadhimisha maadhimisho hayo muhimu.

“Uchunguzi wa sayansi ya Jinai umesaidia kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwa imesadia kubaini wahalifu kirahisi na kuunganishwa na tuhuma zinazowakabili pasina shaka huku wasio na hatia kuachiwa huru,”amesema.

Amesema katika kusherekea siku hii kunaileta jamii pamoja kwani uchunguzi wa kisayansi ni wa kweli ambao husaidia kutenda haki.

Naye Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, DCP. Dk. Lazaro Mambosasa amesema uchunguzi hauruhusu kumuadhibu mtu ambaye hana hatia ambapo amesema uchunguzi wa kisayasi unaleta taswira njema kwa Jeshi la Polisi na Serikali katika kutenda haki.

Kwa upande wake Ofisa kutoka Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa serikali,Fidelis Sekumba amesema uchunguzi wa kisayansi unatoa ushaidi wa uhakika zaidi na kunarahisisha maamuzi ya kisheria kwenye mihimili nayohusika kutoa haki.

Maadhimisho hayo hufayika kila mwaka 20 Septemba yakiunganisha wataalam wa uchunguzi wa kisayasi katika kutanzua uhalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here