Home KITAIFA TASAC YAKABIDHIWA BOTI NA OFISI YA WAZIRI MKUU

TASAC YAKABIDHIWA BOTI NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Dar es salaam

OFISI ya Waziri Mkuu imelitaka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC kushirikiana na Taasisi nyingine za kisekta kuwa na mkakati wa matumizi ya boti katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu majini ikiwemo Uvuvi haramu,usafirishaji dawa za kulevya , biashara za magendo na utoroshwaji nyara za Serikali.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 19,2024 na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dk. Jim Yonazi katika hafla ya Makabidhiano ya Boti ya doria (PB SAILFISH) kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ambapo amesema boti hiyo itatimiza lengo na kuimarisha juhudi za serikali za kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika eneo la bahari na Maziwa Makuu.

Aidha Boti hiyo ilinunuliwa kupitia mradi wa kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa makuu nchini kwa Ufadhili wa serikali ya Japan kupitia shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)

Boti hii kama ilivyoelezwa hapo awali, ilinunuliwa kupitia mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini kwa ufadili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Nitumie nafasi kuwashukuru sana wafadhili wetu hao kwa ufadhili wao na

“Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ina imani kubwa na uwezo wa TASAC katika usimamizi, uendeshaji na utunzaji wa boti hii ndiyo sababu iliyopelekea boti hii kukabidhiwa kwa Shirika hili ni imani yetu kuwa mtaitunza vizuri boti hii ikiwa ni pamoja na kuifanyia matengenezo kwa wakati na na inakwenda kuwaongezea ufanisi katika kazi zenu za kila siku hususani katika ukaguzi kwa meli zinazoingia kwenye maji yetu ya ndani,” amesema Dk.Yonazi

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Ludovic Nduhiye amewasisitiza watumishi wa TASAC watimize wajibu wao mkubwa wa kuisimamia na kuitunza boti hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu ili iweze kuwahudumia wananchi na kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

“Hakikisheni boti hii inasimamiwa na Wataalamu wenye weledi,Taaluma na Uzoefu ili kuhakikisha kuwa boti inatumika kwa mujibu wa miongozo kanuni na taratibu zinazosimamia uendeshaji wa Boti,” amesema.

Pia ameomba TASAC inashirikisha wadau katika kuchangia gharama za uendeshaji wa boti hiyo katika maeneo ya upatikanaji wa mafuta na matengenezo

Kwa upande wake Mkurugenzi Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mohamed Salum amesema kuwa uwepo wa Boti hiyo utasaidia kupambana na vitendo vya kihalifu katika Bahari na maziwa makuu ikiwemo uharamia, usafirishaji wa dawa za kulevya na Binadamu.

Amesema kuwa Boti hiyo itasaidia utekelezaji wa majukumu ya TASAC iliyokasimiwa kisheria, hususani jukumu la usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji mazingira dhidi ya uchafuzi utokanao na shughuli za meli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here