Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI AMEKUTANA NA PRINCESS SOPHIE WA UINGEREZA.

RAIS DK.MWINYI AMEKUTANA NA PRINCESS SOPHIE WA UINGEREZA.

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Uingereza kwamba Zanzibar inaendelea na mikakati na juhudi kubwa ya kuhakikisha inadhibiti na kumaliza ugonjwa wa Trakoma( Trachoma) nchini.

Hayo ameyasema leo Septemba, 19 2024 Ikulu Zanzibar alipozungumza na Princess Sophie (Duchess Edinburgh) ambaye yupo Visiwani humo kwa ziara ya siku sita kutembelea miradi mbalimbali ya afya inayotekelezwa na taasisi tofauti ambazo yeye ji mlezi wake.

Amesema hatua iliyofikia Zanzibar ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali inatokana na juhudi kubwa na misaada ya afya inayotolewa na Uingereza na kumuahidi kuwa Zanzibar itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kupambana na magonjwa yasioambukizwa (NCDs) yanayoathiri ustawi wa jamii.

“Nakuhakikishia Princess Sophie kuwa Zanzibar inaendelea kuweka mkazo zaidi na kuhakikisha huduma bora za sekta ya afya hususan kuimarisha huduma za kitengo cha uzazi salama cha mama na mtoto na amewataka wafadhili pamoja na washirika wengine wa maendeleo kuendelea kuinga mkono Zanzibar, ” amesema.

Kwa upande wake Princess Sophie ameipongeza Zanzibar kwa hatua iliyofikia ya kuthibiti ugonjwa wa Trakoma kwa kiasi kikubwa na kufikia mapema malengo yaliyowekwa na Jumuiya ya Madola(Commonwealth) ya kumaliza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Princess Sophie (Duchess Edinburgh) mke wa mtoto wa mwisho aliyekuwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II, Prince Edward, ambaye ni mdogo wa Mfalme wa sasa Uingereza Charles III.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here