Na Shomari Binda-Musoma
JUMLA ya zahanati 17 zinaendelea kujengwa kwa kasi ndani ya jimbo la Musoma vijijini ili kutoa huduma za afya
Taarifa iliyotolewa leo septemba 17 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema kwa sasa Idadi ya zahanati zilizopo ni 24 za serikali na binafsi 4.
Amesema Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye vijiji 68 linaendelea kuboresha huduma za afya kwa ushirikiano kati ya wananchi na serikali
Ametaja vijiji 17 vinavyoendelea na ujenzi kwa sasa ni Bulinga, Burungu, Butata, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege, Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu ambavyo vyote kasi ya ujenzi unaendelea vizuri.
Amesema zahanati za serikali zipo kwenye vijiji vya Bugoji, Bugunda, Bukima, Busungu, Bwai, Chitare, Etaro, Kiemba, Kigera Etuma, Kiriba, Kome, Kurugee, Kwikuba, Mkirira, Mmahare, Mwiringo, Nyakatende, Nyambono, Nyegina, Rusoli, Seka, Suguti, Tegeruka na Wanyere
“Bado tunaendelea na kasi ya ujenzi kuhakikisha vijiji vyetu 68 vyote vinakuwa na zahanati ili kuendelea kutoa huduma za afya kwa wsnanchi.
Kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi kwenye vijiji 17 kwa ushirikiano wa wananchi na serikali na ujenzi unaendelea vizuri”,amesema
Muhongo amesema licha ya zahanati hizo zinazoendelea kujengwa vituo vya afya 6 vinajengwa kwenye Kata za Bugwema, Etaro (Kisiwa cha Rukuba), Kiriba, Makojo, Mugango na Murangi
Aidha mbunge Huyo amewaomba wadau wa maendeleovwakiwemo wazaliwa wa Musoma Vijijini kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini ukiwemo ujenzi wa zahanati mpya.