Home MICHEZO LAKE VICTORIA FC YASHEREHEKEA MIAKA 60 YA JESHI LA POLISI KWA USHINDI...

LAKE VICTORIA FC YASHEREHEKEA MIAKA 60 YA JESHI LA POLISI KWA USHINDI MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP MUSOMA 2024

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Lake Victoria imesherehekea miaka 60 ya jeshi la polisi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Kamnyonge kwenye mashindano ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024.

Katika mchezo huo uliofanyika leo Septemba 17 kwenye uwanja wa Mara sekondari wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo
wametakiwa kuzingatia nidhamu ili kulinda vipaji vyao.

Ujumbe huo umetolewa na askari Kata wa Kata ya Kamnyonge Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Boniphace Lazaro aliyekuwa mgeni rasmi wa mchezo huo.

Amesema nidhamu ndio njia ya kuweza kufika kwenye mafanikio ya kimichezo kwa mchezaji yoyote.

Lazaro amesema mchezaji yoyote mwenye kipaji kisha akazingatia nidhamu ni rahisi kupata mafanikio na kufika mbali.

Amesema licha ya kucheza kwa nidhamu ni vizuri kila mchezaji kulinda usalama wa mchezaji mwenzake kutokuumizana.

” Tuzingatie nidhamu tunapokuwa uwanjani ili kuvilinda vipaji vyenu na ndio njia itakayowawezesha kufika mbali.

” Kupitia mashindano haya pia tunapeana elimu ya kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa tufanye hivyo kwenye Kata zetu kupitia polisi Kata”,amesema.

Katika mchezo wa leo uliofanyika uwanja wa Mara sekondari timu ya Lake Victoria imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kamnyonge fc.

Mashindano hayo ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024 yataendelea tena kesho kwa mchezo kati ya Ajax fc na Mshikamano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here