Home KITAIFA KIGAHE AMEFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI RUSUMO

KIGAHE AMEFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI RUSUMO

Rusumo

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanayakazi katika mpaka wa Rusumo.

Kigahe ameyasema hayo leo Septemba, 15 2024 alipofanya ziara ya kutemebelea mpaka wa Tanzania na Rwanda ( Rusumo ) kwa lengo kuangalia shughuri za Biashara zinazofanyika katika mpaka huo.

Akiongea wakati wa kujibu taarifa ya utendaji wa kituo hicho kutoka kwa Meneja wa kituo hicho Kigahe amefurahishwa na utendaji wa kituo hicho kwa uchapakazi,uadilifu na kujituma kwa watumishi.

“Nimefurahishwa na taarifa ya kutumia muda machache wa kuvusha magari na watu kwa kutumia dk 32 tofauti na upande wa pili wanaotumia muda mwingi,” amesema Kigahe.

Aidha amesisitiza kuwa soko la kimkakati la Kahaza linalojengwa litakapoanza kutumika lisaidie wakulima kukusanya mazao toka shambani na kuweka lebo kwenye vufungashio ili kuipa thamani bidhaa yetu kutambulika kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake Meneja wa kituo Cha forodha cha Rusumo Amos Illoyo amemshukuru Naibu Waziri kwa kufanya ziara kituoni hapo na kuona shughuri za kibiashara zinavyofanyika.

Ameeleza kuwa Shughuli zinazofanyika katika mpaka huo ni kukusanya mapato ya serikali ,kuthibiti biashara za magendo zinazofanywa maeneo yanayozunguka mpaka ili kuwezesha ulipaji kodi,na kuzuia bidhaa bandia.

Mpaka  wa  Tanzania umekuwa  ni  lango  kuu  la  kupitisha  bidhaa kwenda  nchi  za   Rwanda  na Congo DRC.huku bidhaa  zinazopita  kwa  wingi zikiwa  Cement , vinywaji  baridi.

Naye Afisa Biashara wa wilaya ya Ngara,Privanus Katinhila amesema kuwa kupitia ziara ya Naibu waziri amejifunza mengi ikiwemo maelekezo aliyopewa ya kujikita kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili kazi yake ifanyike kwa weledi.

        

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here