Home KITAIFA DOTTO MAGARI AMEPONGEZA JUHUDI ZA RAIS DK.SAMIA KUHAKIKISHA NCHI INAENDELEA KUWA NA...

DOTTO MAGARI AMEPONGEZA JUHUDI ZA RAIS DK.SAMIA KUHAKIKISHA NCHI INAENDELEA KUWA NA AMANI

Dar es Salaam

MFANYABIASHARA wa magari nchini,Dotto Keto maarufu “Dotto magari” amepoongeza juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani.

Pia amewataka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumuunga mkono Rais Dk.Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

Pongezi hizo Dotto magari amezitoa Septemba 15, jijini Dar es Salaam amesema kuacha siasa za uongo na kumpa Rais Dk. kongole kwa kazi kubwa anayoifanya.

”Nyinyi majirani zetu mlikua hamna ofisi
Kwa takribani miaka 30, leo mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa mikocheni mnataka nini majirani?,”amesema.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” Amesisitiza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here