Home MICHEZO WAFANYAKAZI WA TANESCO PWANI WAFANYA BONANZA LA MICHEZO LA KUPONGEZANA KWA KAZI

WAFANYAKAZI WA TANESCO PWANI WAFANYA BONANZA LA MICHEZO LA KUPONGEZANA KWA KAZI

Pwani

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Pwani wamefanya bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni kwa lengo la kupongezana kwa kazi, burudani za pamoja za kujiimarisha kiafya.

Bonanza hilo lililohusisha Wafanyakazi wa TANESCO mkoa mzima wa Pwani limefanyika lililofanyika katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha Shule ya Sekondari ya Tumbi mjini Kibaha ambapo mashindano yaliyoshindanishwa Wafanyakazi wa TANESCO kiwilaya na Tuzo mbalimbali kwa washindi zimetolewa.

Akizungumza Septemba,14 2024 kwaniaba ya Wafanyakazi hao Afisa Rasilimali TANESCO, mkoa wa Pwani Prescus Mayengo ameitaka Jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yasioambukizwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bonaza hilo Nsanjingwa Samwel pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirik hilo wamesema uwepo wa michezo hiyo imejenga mahusisno mema baina ya watumishi wa shirika hilo na uongozi wao.

Katika bonanza hilo wafanyakazi wa Tanesco mkoa wa Pwani wameshiriki katika michezo mbalimbali iliwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba ,netball, na michezo ya jadi ikiwemo karata, bao, draft, mbio za yai, kuvutana kamba, mbio za kuku na mbio za gunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here