Home BURUDANI DC TANGA AKUTANA NA FAMILIA ZA KING MAJUTO, SHABAN ROBERT.

DC TANGA AKUTANA NA FAMILIA ZA KING MAJUTO, SHABAN ROBERT.

Na Boniface Gideon,TANGA

MKUU wa Wilaya ya Tanga, Raphael Kubecha mwishoni mwa wiki hii amekutana na familia za wanasanaa maarufu nchini King Majuto na Shaban Robert amekutana na familia hizo kwalengo la kutoa msaada wa vyakula pamoja na kuweka mikakati ya namna ya kuwaenzi wanasanaa hao maarufu nchini,ambapo alionesha kutokufurahishwa na uchakavu wa maktaba ya kazi za mwanzilishi wa lugha ya Kiswahili nchini.

Kubecha aliziomba familia hizo ambazo ni ndugu ,kukaa kwapamoja na kutoa mpango kazi ambao utasaidia kujenga makta za kumbukumbu hususani kwa mwanzilishi wa lugha ya Kiswahili nchini Shaban Robert.

“Niwaombe nyie kama familia,fanyeni kikao alafu mlete mpango kazi ambao utasaidia tujenge makta nzuri hapa kwenye makazi ya hayati Shaban Robert,tunataka tuwaenzi kwa vitendo,zoezi la ujenzi wa makta utaenda sambamba na tamasha ambalo litawakutanisha wadau mbalimbali,na tutaangalia katika tamasha letu lifanyike siku moja wapo kati ya siku ya kuzaliwa au kufariki kwake”amesisitiza Kubecha

Amesema Serikali ya Wilaya hiyo imepanga kuwaenzi kwavitendo watu wote waliotoa mchango mkubwa katika jamii kupitia sekta mbalimbali pia itaweka mifumo ya utalii kupitia kazi zao.

“Tukijenga makta nzuri,tuje tuweke kazi zao,mfano Mzee Shaban Robert alikuwa ndio mwasisi wa kuvaa vazi la kanzu,koti la suti na barakashee,lakini pia mwanzilishi wa lugha yetu ya kiswahili, kupitia yeye Kuna watu ni maprofesa kupitia kazi za Shaban Robert,kwahiyo ni lazima tumuenzi kwa vitendo ili kizazi kiendelee kujifunza mema yote aliyotuachia,”amesema Kubecha

Naye Paskal Mbunga mdau wa sanaa na Mwandishi wa habari aliyebobea katika sanaa na lugha,alipongeza wazo hilo la kuwaenzi kwavitendo watu wote waliotoa mchango mkubwa katika jamii kupitia kazi zao,

“Mimi nikiwa Mwandishi wa habari na pongeza sana wazo hili,na tunamuomba mkuu wa Wilaya alitekereze kwa vitendo ili liweze kuleta hamasa kwa vizazi vijavyo,mimi mwenyewe nimekuwa mbobezi kwenye sanaa ya lugha lakini chanzo ni Shaban Robert, kwahiyo naomba sana Serikali ilitekereze wazo hili kwa vitendo,”amesisitiza Mbunga

        

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here