Home KITAIFA BASHE: SIKIMU YA MZEE SHIJA KUNUFAISHA WAKULIMA WA WILAYA YA KAHAMA

BASHE: SIKIMU YA MZEE SHIJA KUNUFAISHA WAKULIMA WA WILAYA YA KAHAMA

Shinyanga

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga leo Septemba15, 2024 ambapo ametrmbelea mradi wa bwawa la umwagiliaji lililopo katika kijiji cha Malenge, Kata ya Isagehe lenye ukubwa wa mita za ujazo wa 600,000 kwa thamani ya shilingi bilioni 2.5.

Bwawa litakuwa na mifereji mikuu na midogo ya kuingiza maji mashambani yenye urefu wa jumla wa kilomita 13 , pamoja na eneo litakalotengwa kwa ajili ya kunywesha mifugo. Mradi unatekekellezwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Serikali.

“Naielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Barrick kufanya usanifu utakaowezesha kuongeza eneo la hekta 400 ili wakulima zaidi ya 427 wanufaike na mradi na kuwa na kilimo cha uhakika cha kuvuna hadi mara tatu kwa mwaka”, amesema.

Waziri Bashe pia amemshukuru Mzee Shija Lukinga ambaye ni mmiliki aliyetoa eneo lake la ardhi bure ili kupisha mradi huo.

“Hii ni taswira chache ya Mzee Shija kujitolea na ni kipaji cha kipekee. Naielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji isajili skimu hii kwa jina la Mzee Shija,” amesema.

Aidha, Waziri Bashe amewashukuru pia Kampuni ya Uchimbaji Migodi ya Barrick kwa kuwezesha mradi huo.

“Sisi kama Serikali tutakamilisha usakafiaji wa kilometa 12 zilizobaki na Serikali itajenga hekta 400 za tuta zilizobaki,” ameongeza.

Ameeleza pia kutajengwa Kituo cha Zana za Kilimo na ujenzi wa maghala kwa ajili uhifadhi wa mpunga.

“Ninamuomba Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kufanya kikao cha ujirani mwema na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili bonde la Manonga lilindwe kwa ajili ya miundombinu ya uzalishaji wa chakula badala ya kujenga nyumba za wakazi. Tulinde ardhi ya kilimo,” amesema Waziri Bashe.

Aidha, amewafikishia wakazi wa Kata ya Isagehe salamu za Rais Dk. Samia kwa kueleza kuwa dhamira yake ya kukuza kilimo ni ya kudumu na ataendelea nayo katika kuinua hali ya wakulima nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here