Home KITAIFA TANZANIA INAUNGANA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA TABAKA LA UZONI.

TANZANIA INAUNGANA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA TABAKA LA UZONI.

Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Dk. Ashatu Kijaji  amesema Tanzania inaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Uzoni.

Akizungumza leo Septemba14, 2024 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari Dk. Kijaji  wakati amesema Tabaka la Uzoni kazi yake kubwa kuchuja sehemu kubwa ya miozi ya jua isifike kwenye uso wa dunia .

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika Septemba 16,2024 jijini Dodoma na hiyo ni kama kumbukumbu ya kukumbuka tarehe ya kutiwa saini Itifaki ya Montray ya mwaka 1987  kuhusu kemikali zinazomomonyoa Tabaka la Uzoni huku wizara hiyo imejipanga kutoaelimu kwa mafundi majokofu na viyoyozi jijini humo.

“Kauli mbiu ya siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Uzoni kwa mwaka 2024 ni “Itifaki ya Montray kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi” ,kauli mbiu hiyo imechagauliwa ili kuendelea kulinda uelewa kwa umma na kwa namna ambavyo Itifaki hiyo imechangia katika hifadhi ya Tabaka la Uzoni na kuwa nyenzo muhimu katika kuchangia jitihada za kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi,” amesema.

“Tabaka la Uzoni linapoharibiwa linaruhusu mionzi ya jua kufika moja kwa moja kwenye uso wa Dunia na kusababisha kuongezeka kwa magonjwa mbalimbali kama saratani ya ngozi ,mtoto wa jicho ,upungufu wa kinga mwilini, na kujikunja Kwa ngozi,”amesema

Amesema Madhara mengine ni pamoja na kuathirika wa ukuaji wa mimea ,na baadhi ya kemikali hizo kusababisha kuongezeka kwa joto duniani na Kuchangia katika mabadiliko ya Tabia ya nchi .

“Kemikali hizi ni zile ambazo zinatumika katika majokofu ,viyoyozi ,vifaa vya kuzimia moto ,usafishaji chuma ,utengenezaji magodoro ,ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na kilimo cha maua ,hifadhi ya nafaka katika maghara,”amesema Dk.Kijaji.

“Tukiwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya kimataifa kwa mwaka 2023 kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kushirikiana na wadau mbalimbali iliadhimishwa siku hii ya hifadhi ya Tabaka la Uzoni kwa kutoa elimu kwa umma ,mafunzo ya kudhibiti uingizaji wa kemikali ,elimu kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kulinda Tabaka la Uzoni.

Ameongeza kuwa katika kuadhimisha siku ya Tabaka la Uzoni kwa mwaka huu Serikali imepanga kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ,ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu makala mjongeo  la Tabaka la Uzoni kuendelea kuelimisha jamii kupunguza shughuli mbalimbali za kibinadamu ,kutoa elimu kwa mafundi  viyoyozi na majokofu katika Jiji la Dodoma kuhusu namna bora ya kukarabati vifaa hivyo pasipo kuachia angani kemikali zilizotajwa. 

Pia ametoa  rai kwa watanzania kushiriki katika Tabaka la Uzoni ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi kwa kupunguza kuepuka kuingiza  Gesi zilizopigwa marufuku, vifaa vinavyotumia Gesi vilivyoharibika kama vile majokofu ,viyoyozi vilivyotumika (mitumba ) kuendelea kununua bidhaa zenye nembo sahihi, kutupa ovyo majokofu, na vifaa vingine vinavyosababisha Tabaka la Uzoni nchini

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here