Home KITAIFA RAIS DK.MWINYI: AMESISITIZA KUSIMAMIA IPASAVYO SEKTA YA UVUVI NA MAZAO KUIMARISHA UCHUMI

RAIS DK.MWINYI: AMESISITIZA KUSIMAMIA IPASAVYO SEKTA YA UVUVI NA MAZAO KUIMARISHA UCHUMI

Dar es Salaam

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amefungua mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya uvuvi na utanzaji wa viumbe Maji wa nchi za Afrika karibia na Pasifiki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Septemba,13 2024 Dk.Mwinyi wakati akifungua mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere amezisisitiza nchi wanachama kuendelea kusimamia ipasavyo sekta ya uvuvi na mazao ya bahari kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.

Ameelezea kuwa mradi wa FiSHCAAP, ulioendeshwa katika nchi 12 kwa mafanikio makubwa kuwa nyenzo muhimu ya kupunguza uvuvi usio sahihi na uvunaji mazao ya bahari.pamoja na kubadilisha mitazamo ya kiuchumi ya jamii katika nchi husika.

“Wakati umefika wa kuunganisha nguvu za pamoja, mbinu na maarifa yaliyopatikana kupitia mradi huu ili kuimarisha sekta ya uvuvi pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa za mazao ya bahari,” amesema.

Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kasi ya ongezeko la watu katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara inabainidgq kuwa mahitaji makubwa ya samaki kwa miaka ijayo hivyo yanayohitaji usimamizi endelevu wa bahari.

Ameongeza kuwa Tanzania kupitia mpango mkuu wa sekta ya uvuvi wa mwaka 2021 hadi 2037 na mpango mkuu wa uvuvi Zanzibar wa mwaka 2023 hadi 2038 pamoja na mpango mkuu wa Taifa wa utekelezaji imejipanga kuwa endelevu na yenye ufanisi katika kusimamia sekta ya uvuvi na mazao ya bahari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here