Home KITAIFA HESLB WABADILISHANA HATI YA MAKUBALIANO NA TRA

HESLB WABADILISHANA HATI YA MAKUBALIANO NA TRA

Dar es salaam

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato TRA imeingia makubaliano ya kubadilishana hati ya ushirikiano kwa ajili ya kurahisisha ukusanyaji madeni kwa wanufaika wenye kipato ambao hawajarejesha .

Akizungumza leo Septemba 13,2024 Jijini Dar es salaam katika hafla hiyo ya makabidhiano ya hati ,Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dk.Bill Kiwia amesema kuwa lengo la kushirikiana na TRA ni kuwafikia wanufaika wa mikopo walio katika sekta isiyo rasmi ambao wana kipato na hawajarejesha mikopo yao.

“Ushirikiano huu HELSB unakwenda kuboresha huduma kwa urahisi kuweza kuwafikia wanufaika wa mikopo kupitia kanzidata za TRA ambao watatoa taarifa zao za shughuli wanazozifanya wakiwa wanalipa kodi hivyo watabainika hapo na kuanza kufuatiliwa na ambao watakuwa wakaidi na hawajairejesha tutawachukulia hatua ili wanufaika wengine walio vyuoni nao waweze kunufaika kama walivyonufaika wao,” amesema.

Amesema jambo wanalolifanya litachangia sisi HESLB na TRA kubadilishana uzoefu baina yao na kuwafanya wale wasiorejesha mikopo yao ambao hawapo kwenye ajira rasmi lakini wana kipato kupitia sekta isiyo rasmi,kurejesha Mikopo

Aidha ametoa wito kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao bado hawajaanza kurejesha Mikopo yao,kurejesha kwa wakati ili kufanya bodi hiyo kuwa na uwezo wa kutoa Mikopo kwa Wanufaika wengine.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Yusuph Mwenda mikopo hiyo inayotolewa.ni kodi za watanzania hivyo bodi imekuwa ikikabidhiwa fedha ili kuwapatia waombaji wa mikopo hivyo watanzania waendelee kulipa kodi kwa uaminifu .

“Watanzania napenda mfahamu kuwa hiki kinachofanywa na Bodi ya Mikopo kwa. Wanafunzi wa Elimu ya juu ni Matokeo yenu ya kulipa Kodi na hatimaye kodi hizi pia kutumika kugharamia bodi katika utoaji mikopo kwa watoto wetu wa kitanzania,” amesema Mwenda.

Aidha Kamishna Mwenda amesema kuwa TRA itakuwa mstari wa mbele kubadilishana taarifa na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu(HESLB) ili kuhakikisha wanufaika wa mikopo ambao wako sekta isiyo rasmi wanarejesha mikopo hiyo.

HELSB imekua ikishirikiana na wadau mbalimbali wa Kimkakati ili kuhakikisha wanaleta ufanisi mkubwa katika utoaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu kwa Watanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here