Home KITAIFA UWEPO WA SGR UNAASHIRIA UTOSHELEVU WA UMEME NCHINI – DK. BITEKO

UWEPO WA SGR UNAASHIRIA UTOSHELEVU WA UMEME NCHINI – DK. BITEKO

đź“ŚAsema Nishati ya Umeme ya Uhakika Yafungua Fursa za Uchumi

đź“ŚNjia Kubwa Zaidi ya Umeme Kujengwa Kutoa Umeme JNHPP hadi Dodoma

Dar es Salaam

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko amesema safari za treni za reli ya kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dk. Biteko ameyasema hayo leo Septemba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa mara ya kwanza.

“Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka,”amesema Dk. Biteko

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha umeme unatosheleza Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here