Home KITAIFA SHIUMA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YAO

SHIUMA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YAO

Na Magrethy Katengu -Dar es salaam

SHIRIKISHO la Umoja wa Wamachinga Tanzania(SHIUMA) kufanya mabadiliko ya Katiba katika Mikoa yote Nchini ili kuweza kuondoa mapungufu mengi yaliyomo kwani imesababisha baadhi ya Vyama vya Wamachinga kushindwa kujiunga na Shirikisho hilo nakufanya washindwe kufikia Malengo yao.

Hayo yamebainishwa Septemba 11,2024 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Umoja huo Steven Lusinde wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoa maadhimisho ya Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi za Mikoa waliyokutana Jijini Dar es salaam.

Aidha pamoja na Mambo Mengine Lusinde amesema kuwa Katiba iliyopo imekua na mapungufu huku akitoa maagizo kwa Wenyeviti wa Vyama vya Wamachinga kote Nchini kuhakikisha wanatekeleza Makubaliano ya kufanya Marekebisho ya Katiba hiyo,nakujiandaa kwa Uchaguzi wa Viongozi wa SHIUMA Taifa utakaofanyika Mwezi Februari 2025.

“Tumeunda Kamati maalumu kutoka Vyama 15, ambapo Dar es salaam Vyama vitatu na Vyama vingine vinatoka kwenye Mikoa mingine,hii ni hatua ya kuboresha Katiba yetu ambayo ilikua inatufanya tuyumbe,” amesisitiza Lusinde

“Kuna barua ya tarehe 22 ,7 ,2024 kutoka kwa msajiri wa Vyama vya uraia Tanzania,ambaye alitutaka tufanye Marekebisho ya Katiba yetu,hiyvo tuna muda wa miaka mitatu ya kufanya Marekebisho ya Katiba ,na sio kunandika Katiba mpya,” amesema.

Aidha amesema kuwa suala jingine walilodhamiria Viongozi hao ni kutatua Migogoro inayojitokeza baina yao na kutengeneza Umoja wao,kwani serikali ya Rais Samia inawajari Wamachinga hivyo hawawezi kumwangusha Rais Samia DKt Samai Suluhu Hassan.

Jambo jingine ni ukataji wa kitambulisho Cha Ujasiliamari ambacho ni muhimu katika Utekelezaji wa majukumu yao ,hivyo Lusinde amewahimiza wa machinga wote Nchini kununua kitambulisho hicho kwa manufaa ya kazi yao.

“Tukipata Kitambulisho cha Ujasiliamari kitatusaidia,saivi tunaenda kuanzisha SACCOS zetu ngazi za Mkoa ,kwani taaisis hizi ndizo muhimu katika kazi zetu,hivyo natoa maelekezo kwa Viongozi wa Wamachinga wote Nchi nzima wahakikishe wanaanzisha SACCOS katika Mikoa yao,”amesema

Pia Lusinde amebainisha kuwa Wamachinga wapo tayari kulipa Kodi,kutokana na hivi karibuni kukutana na kamishna wa Mamlaka ya Mapato Nchini( TRA) nakukubaliana kwa pamoja namna ya ulipaji wa Kodi hiyo huku wakiomba kutengeneza Mazingira rafiki ya kufanyia Biashara zao.

“Tutahakikisha tunamsaidia Kamishna wa TRA kuchangia pato letu kwenye pato la Taifa,tupo tayari kuchangia pato la Taifa kulingana na kipato chetu tunachopata.amesisitiza.

“Tumeona mfumo wa Rais wa Maridhiano( 4R) unatugusa hata sisi wamachinga ,hivyo tutachangia pato la Taifa lakini tunaomba kuhakikishiwa Mazingira mazuri ya kufanya biashara,”ameongeza.

Katika hatua nyingine Umoja huo wa Shirikisho la Wamachinga Tanzania umeishukuru serikali kwa kuwajengea Ofisi za Wamachinga kila Wilaya na Mikoa ili kurahisisha utendaji kazi.

Amewahimiza Wamachinga Kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki ipasavyo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba Mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu Mwakani.

“Shirikisho la Wamachinga ni huru,nakwamba wanaopita huku na kule kuwagombanisha na Serikali hawako tayari kuyumbiswa na mtu nakwamba silaha yao kubwa ni kufanya Biashara ili kuunga mkono Maendeleo ya Taifa.

“Kuanzia leo Vyama Vyote kutoka Mikoa 26 tunahakikisha vimesajiliwa ,hivyo leo tunagawa rasimu za Katiba ili kila Mkoa uweze kupata Katiba na kuweza kusajiliwa nakufanya Shirikisho la Wamachinga kuwa imara zaidi,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here