Home KITAIFA HESLB KUSHIRIKIANA NA TAASISI TATU KUWASAKA WADAIWA SUGU WA MIKOPO.

HESLB KUSHIRIKIANA NA TAASISI TATU KUWASAKA WADAIWA SUGU WA MIKOPO.

Dar es Salaam

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Imebadilishana hati za makubaliano na Taasisi tatu za kimkakati ambazo zinaenda kutekeleza kwenye utoaji wa taarifa katika kuwasaka wadaiwa sugu wa mikopo ambao walipewa kipindi wako vyuoni na kushindwa kurejesha kwa wakati.

Taasisi hizo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), CREDITINFO Tanzania Ltd ambayo ni taasisi ya uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo katika taasisi za fedha.

Hayo yamesemwa Septemba, 11 2024 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji waHESLB, Dk. Bill Kiwia amesema kuwa lengo la kubadilishana hati za makubaliano na taasisi hizi ni kuweza kuongeza mbinu ya kuwapata wadaiwa sugu wa mikopo hiyo hususani wale walioko kwenye sekta binafsi na isiyo rasmi kwa matumizi ya mifumo ya tehama.

“Bodi ya mikopo inatoa rai kwa wanufaika wa mikopo Hiyo ambayo walipewa ili waweze kurejesha mikopo kwa wakati ili wengine waweze kwenda vyuoni kuendelea na masomo huku Taasisi Ya Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), wakala wa usajili ,ufilisi na udhamini RITA,taasisi za uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye taasisi za fedha CREDITINFO zikiwa tayari kwa majukumu ya kuwasaka wadaiwa hao,” amesema.

Ameongeza kuwa katika ukusanyaji wa mikopo hiyo tunawakaribisha wadau hawa katika kwenda kufikisha ujumbe huu kwa kutumia Mifumo ya tehama.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Deusdedit buberwa amesema kuwa watashirikiana vyema katika kutekeleza makubaliano ya serikali huku taasisi za kiserikali zikiweza kuunganisha mifumo ya katika kutoa huduma kwa wananchi.

Naye Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank kanyusi amesema kuwa wana jukumu la kutoa vyeti vya uzazi na Vifo katika kuweza kukamilisha suala hilo la wadaiwa hivyo wao kama RITA wameweza kujiunga na mfumo wa kieletronik ili kumwezesha kupata Cheti ambapo HESBL watahitaji kuona vyeti vya muombaji wa mkopo ili kuhakikisha kuwa ana visibitisho vyote .

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa CREDITINFO, Edwin Urasa ameongeza kuwa wanufaika wa mikopo hiyo ya elimu ya juu waanze kujitokeza na kurejesha mikopo kwa wakati sahihi ili taasisi za fedha ziweze kukopesha wanavyuo wengine ambao wanatarajia kwenda vyuoni hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here