Home KITAIFA WAZIRI WA VIWANDA SELEMAN JAFO AKIZINDUA MAONESHO YA CHEMBA YA WAFANYABIASHARA MWANZA

WAZIRI WA VIWANDA SELEMAN JAFO AKIZINDUA MAONESHO YA CHEMBA YA WAFANYABIASHARA MWANZA

Mwanza

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Seleman Jaffo ameitaka chemba ya Biashara, Vwanda na Kilimo (TCCIA) kuanza maonesho hayo kwa ngazi ya kitaifa kwa bidhaa na huduma wanazozalisha ndani ya Afrika Mashariki.

Dk.Jaffo ameyasema hayo Septemba, 10 2024 Jijini Mwanza katika uzinduzi wa maonesho ya 19 ya TCCIA ambapo wadau mbalimbali toka Jukwaa la Biashara, Viwanda na Kilimo wa eneo lote la Afrika Mashariki.

Amesema maonesho hayo yana tija zinazowawezesha wadau hao kubadilishana uzoefu, maarifa na kujenga mahusiano ya watu wa ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na nguvu.

“Natamani kusikia wafanyabiashara toka mataifa mengine hawarudi na bidhaa zao kwani hapa nchini kuna soko la vitu hivyo muwe na mikataba ya kibiashara,”amesema Dk.Jaffo.

Ameongeza kuwa hatua ya kuimarisha mashirikiano itawawezesha kufanya biashara hata kupitia Mpango wa Kukuza na kuongeza Fursa (AGOA) unaoruhusu bidhaa mbalimbali kuingia bila vikwazo nchini Marekani na soko la Afrika.

Naye Makamu wa Rais wa TCCIA, Boniface Ndengo ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha ulinzi wa mitaji yao chini sera nzuri aliomba iharakishwe jitihada ya kuwepo kwa mazingira rahisi ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Amesema wanadhamiria ya kuuza bidhaa zao katika soko la Afrika hivyo mazingira ya ulipaji kodi yaongeze kasi ya wafanyabiashara kutokuwa waoga kufanya biashara kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.

Kwa upande Mkrugenzi Mtendaji wa Mohpans Herbal Medicine & Nutritional Supplements, Profesa Wanfoko Henry toka nchini Uganda mshindi kwenye maonesho hayo, amesema anashukuru kuwepo kwa tukio hilo kwani inawapa fursa ya kuuza bidhaa zao za dawa katika soko hilo na kusaidia kufundisha utengenezaji wa dawa.

Amesema tiba Asili ina umuhimu kwa waafrika kwani inasaidia kuponesha magonjwa mbalimbali ambayo yanawafanya watu kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali katika maeneo yao.

Hilda Massam wa PH Selection mshindi wa maonesho hayo toka nchini Tanzania amesema tiba Asili wanazozalisha zinasaidia katika kufanya ngozi kurudia katika ubora wake wa awali.

Amesema fursa hiyo ya biashara na mataifa ya Afrika Mashariki inawasaidia vilevile kujua ubora wa dawa wanazotengeneza hapa nchini.

Mkrugenzi Mtendaji TJM Product, Teddy Mkamimshindi wa tuzo hizo toka Tanzania mkazi wa Jijini Mwanza, alisema anatamani kauli mbiu ingekuwa “Afrika Tunaweza” amesema dawa zake ambazo tiba lishe zinaonesha mafanikio makubwa.

Amesema dawa za kiafrika zina matokeo chanya na hilo limejidhihirisha kipindi Cha UVIKO19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here