Home KITAIFA WANAFUNZI 62,214 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA 7 MKOA WA MARA KESHO

WANAFUNZI 62,214 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA 7 MKOA WA MARA KESHO

Na Shomari Binda-Musoma

JUMLA ya Watahiniwa 62,214 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wa utakaoanza kesho septemba, 11 2024.

Akizungumza na leo Septemba,10 2024 na Lajiji Digital ofisini kwake Katibu Tawala mkoa wa Mara Gerald Kusaya amesema kati ya wanafunzi hao wavulana ni 29,424 na wasichana ni 32,790.

Amesema wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba kwenye shule 876 ambazo zitakuwa ni vituo vya mtihani.

Kusaya amesema wanafunzi hao ni wale walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2018 na wanakamilisha mzunguko wao wa kielimu wa miaka saba mwaka 2024 na watakuwa kwenye mikondo 2,756

Katibu Tawala huyo amesema mwaka huu Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA) limefanya maboresho mapya kwa mwaka 2024 tofauti na yaliyofanyika 2023 ambapo mtihani wa kuhitimu darasa la saba utajibiwa kwenye karatasi za maswali.

Amesema hiyo imetokana na Baraza hilo kufanya mabadiliko ya utunzi wa mitihani kwa kufuata mtindo mpya ( Format) hivyo hakutakuwa na OMR za kujibia.

” Mitihani hii itafanyika kwa siku 2 septemba 11 na 12 na kwa mkoa wa Mara maandalizi yote tayari yamekamilika na mitihani imefika vituo husika.

” Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi tunawatakia wanafunzi wote mtihani mwema kuanzia hapo kesho,”amesema.

Aidha Katibu Tawala huyo amewataka wanafunzi na wasimamizi kujiepusha kufanya udanganyifu wowote ili kujiepusha na matatizo ikiwemo kufutiwa matokeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here