Home KITAIFA DK. BITEKO AMFARIJI ANGELAH KAIRUKI

DK. BITEKO AMFARIJI ANGELAH KAIRUKI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 10, 2024, amesaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa Mzee Peter Orgones Mkwizu, Baba wa Mhe. Angelah Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum na Mshauri wa Rais.

Dk. Biteko amefika nyumbani kwa Kairuki, Tegeta, Jijini Dar es Salaam kufuatia msiba huo uliotokea Septemba,9 2024 katika Hospitali ya Lugalo alipokuwa akipatiwa Matibabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here