Home KITAIFA FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE WAPATA AJIRA.

FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE WAPATA AJIRA.

Na Sophia Kingimali.

CHUO cha Ufundi Stadi Furahika(VETA) wanatoa rai kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata elimu katika chuo hicho kwani asilimia 75 ya wahitimu wa chuo hicho wamepata ajira katika maeneo mbalimbali yakiwemo utalii na hotel.

Pia,Chuo kinatarajia kufanya mahafali Septemba, 28 2024 ili kuwaanga wanafunzi wanaombaliza na kuingia kwenye soko la ajira ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza Spetemba, 7 2024 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari Kaimu Mkuu wa chuo hicho Dk. David Msuya amesema wahitimu wanaotarajiwa kuagwa ni wale waliopo kwenye mfumo wa elimu bure ambayo inatolewa chuoni hapo.

“Wanafunzi wetu wanaohitimu ni wale waliokuwa kwenye mfumo wa elimu bure ambapo wanachangia kiasi cha shilingi 50000 tu kama gharama za mitihani yao ni hii inawezeshwa na serikali yetu lengo likiwa kugakikisha kila kijana nchini anapata ujuzi utakao msaidia kuondokana na utegemezi unaopelekea kuingia kwenye makundi maovu,”amesema Dk. Msuya.

Aidha amewataka wazazi kujitokeza kwenye mahafali hayo na kuwakaribisha wengine ili waje wajionee namna ambavyo vijana wanavyoweza kujikomba kiuchumi kwani wanapomaliza hapo wanauwezo wa kujiajili na kuajirika ambapo pia chuo kinachukua nafasi kubwa katika kuhakikisha vijana hao wanapata nafasi ya kufanyakazi katika taasisi mbalimbali kutokana na taaluma zao.

Dk. Msuya amesema kuwa katika harakati wanazozifanya za kutokomeza ukatili wanatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo Zanzibar huku akitoa rai kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwafadhiri ili waweze kufikia lengo lao la kuhakikisha elimu ya ukatili inawafikia kila mtu hasa waliopo pembezoni.

Amesema wamekuwa wakijitolea kutoa elimu ya ukatili katika makundi ya watu mbalimbali hasa waliopo vijijini lakini changamoto kubwa inayowakwamisha ni jinsi ya kuwafikia wahusika kwani zaidi wanajiwezesha wenyeshe na kushirikiana na ofisi ya Maendeleo ya Jamii.

“Malengo yetu ni kuhakikisha elimu ya ukatili inawafikia wahusika wengi zaidi hasa waliopo vijijini kwa asilimia kubwa ndio waathirika wakubwa wa ukatili huo,lakini tunachangamoto nyingi zinazotukwamisha na ndio maana tunaomba wadau wajitokeze kutusaidia hata wakitupa gari hata kama ni bovu sisi tutarekebisha kwani litakuwa limetusaidia kuwafikia wahusika wetu,”amesema.

Pia,Dk. Msuya ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaunga mkono lakini pia chama cha Mapinduzi CCM kwa kuendelea kuhakikisha watoto waliopo kwenye maeneo yao wanawapeleka chuoni hapo kupata elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here