Dar es Salaam
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoa amesema tangu mwanaea afariki dunia hajawahi kuangalia filamu ya Kanumba hata moja kwa sababu zinamuumiza.
Pia amepongeza waandaji wa Tamasha la Faraja ya Tasnia kuwakumbuka wasanii mbalimbali wa filamu,Muziki na Waandishi wa Habari lililojulikana kama Faraja ya Tasnia kitendo hicho kimeweza kuwagusa na kuwakumbusha mazuri na mema waliyoyafanya katika tasnia na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema leo Septemba 7,2024 jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders ambapo Tamasha la Faraja ya Tasnia 2024 lengo likiwa ni kuwaenzi wasanii wote ambao wametangulia mbele za haki na Kanumba ni miongoni mwa wasanii hao
”Leo ni siku muhimu kwangu kabla ya kuja hapa nilivyoamka nimelia sana namkumbuka mwanangu lakini niombe tamasha kama hili liendelee kwani inasaidia hawa watu kubaki kwenye mioyo ya wapendwa wao na Leo ni siku ya faraja kwani Bado anamkumbuka mwanae hadi Leo,”amesema mama kanumba.
Ameongeza kuwa kuwa walioofikiria kuja na tamasha hilo wamefanya jambo jema kwani kuwaenzi wasanii na wengine walio kwenye tasnia ni moja ya njia ya kuonesha kuwa watu hao bado wanathamini wa jamii.
Kanumba ametimiza miaka 12 tangu kifo chake ambapo alifariki dunia Aprili, 7 mwaka 2012 na miongoni mwa filamu amewahi kutamba nazo, uncle Jj, This is it, Big Daddy, Deception , She is my Sister na zingenezo.
Kwa upande wake Msanii wa Maigizo nchini Vaileth malle(Mama Afrika) amesema kumbukumbu hiyo imekuwa ya historia kwao kwani wameweza kuwakumbuka wanatasnia lakini pia wataendelea kuyaenzi yale yote mazuri waliyoyafanya.
Tamasha la Faraja ya Tasnia limeandaliwa na wasanii wote kwa ujumla limeudhuliwa na viongozi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki zaidi ya 230 wametangulia
Zadi ya wasanii 230 wametangulia mbele ya haki na Miongoni mwa wanatasnia wanaoenziwa kwenye tamasha hilo ni pamoja na Marehemu Albert Mangwair,Amina Chifupa,Mzee Matata,James Dandu(mtoto wa Dandu),Ruge Mutahaba,Mzee Majuto,Sajuki,Godzilla,Sharo Milionea,Kibonde,Mandojo,Gardner G Habash,Remi Ongala,Maunda Zorro,Captain Komba,Bi Kidude,na wengine.