Home KITAIFA KIKWETE AMETOA WITO KWA WAHITIMU WOTE NCHINI KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI.

KIKWETE AMETOA WITO KWA WAHITIMU WOTE NCHINI KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI.

Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa wahitimu wote nchini kutumia fursa zinazotolewa na Serikali kupitia program za Elimu, Mafunzo na Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa kutoa mikopo na mitaji fursa za ajira rasmi na zisizo rasmi katika miradi ya Serikali inayopatikana katika Wizara za kisekta na sekta binafsi.

Ridhiwani, amesema hayo leo Septemba 7,2024 wakati akijibu swali la Amina Ally Mzee Mbunge wa Viti Maalum, Bungeni leo jijini Dodoma.

“Kuwezesha vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuwa na uzoefu wa kazi pamoja na sifa nyingine za kujiajiri ndani na nje ya nchi, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Program mbalimbali za mafunzo ya Uzoefu wa kazi ikiwemo Internship, mafunzo ya Uanagenzi na utekelezaji na usimamizi wa maboresho yaliyofanywa ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambayo inatambua na kuhimiza uwezo wa mfumo endelevu wa kuwajengea uwezo vijana na stadi mbalimbali ili waweze kuajirika,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here