Home KITAIFA GST NA KIGAM YAANZA MAJADILINO YA AWALI KUHUSU TAFITI ZA MADINI MUHIMU...

GST NA KIGAM YAANZA MAJADILINO YA AWALI KUHUSU TAFITI ZA MADINI MUHIMU (CRITICAL MINERALS)

Dodoma

SERIKALI ya Tanzania kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza majadiliano ya awali kuhusu mashirikiano na Serikali ya Korea Kusini kupitia Taasisi ya Jiosayansi na Rasilimali Madini (KIGAM) kwenye tafiti za Madini Muhimu (critical minerals) nchini Tanzania.

Majadiliano hayo, yamefanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia Septemba 5 hadi Septemba 6, 2024 jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo ni matunda ya ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Korea Mwezi Juni mwaka huu ambapo Tanzania na Korea zilitia Saini Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano katika nyanja za Utafiti na Uongezaji thamani madini nchini.

Aidha, Majadiliano hayo yamehusisha Wataalamu wa Jiolojia kutoka Taasisi ya KIGAM ya nchini Korea na Waatalamu wa Taasisi ya GST ya nchini Tanzania yakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia Dk. Ronald Massawe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here