Dar es Salaam
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wabunifu wa maumbo na alama za bidhaa kusajili kazi zao ili kuweza kutambulika kitaifa na kimataifa.
Akizungumza na wanahabari Leo Septemba 5,2024 Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Godfrey Nyaisa amesema hatua hiyo itawawezesha wamiliki bunifu kuweza kutambulika na kujulikana kwenye biashara zao.
Amesema kuwa lengo la mkutano huu wa siku ya leo nikutakakujadili sheria ya maumbo bunifu kwenye bidhaa ili kulinda alama za biashara zao zeweze kujulikana kitaifa na kimataifa.
“Kifungu hha Sheria cha Mwaka 1974(76) kimebainisha kuwa usajili wa miliki bunifu ni muhimu kwa biashara hususani bidhaa zinazoingia ndani ya nchi na nje ya nchi,”amesema.
Ameongeza kuwa usajili wa alama na miliki bunifu kutarahisisha wafanyabiashara kuuza bidhaa zao zinazohitaji nje ya nchi na ndani ya nchi.
Amebainisha kwamba kumekuwa na changamoto ya wabunifu na wafanyabiashara kutoa vifungashio vyenye ubora na vinavyofanana jambo ambalo ubunifu umekua mdogo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa BRELA Zanzibar Mustafa Haji amesema sekta ya wabunifu inayo mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema PPRA na BRELA wanamchango mkubwa katika kusimamia miliki bunifu ili ziweze kuleta mafanikio ya kukuza uchumi wa nchi.